Joy FM
Joy FM
1 December 2025, 16:25

Wazazi wanapofuatilia maendeleo ya watoto wanaweza kugundua mapema kama mtoto ana matatizo ya kitaaluma, kitabia, au kihisia ili changamoto zikibainika, ni rahisi kupata suluhisho kabla hazijawa kubwa na ushiriki wa mzazi umethibitishwa kuwa na athari chanya kwenye matokeo ya mtoto shuleni, ikiwemo kujiamini, nidhamu, na uwezo wa kujitegemea.
Na Prisca Kizeba
Wazazi na Walenzi Manispaa ya Kigoma Ujiji, wameaswa kuendelea kuwasaidia watoto wao na kufuatilia maendeleo yao shuleni.
Hayo yamesemwa na Mkurugernzi wa shirika la joy in the harvest Mwenge Munyombi wakati wa sherehe ya mahafali ya tatu ya watoto wa shule ya awali Kembridge Share na kuwa wazazi wanao wajibu wa kufuatilia maendeleo ya mtoto wake ili kufahamu mienendo yake.

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa shule hiyo Bi. Betha Silvest Bugaga ameleza namna wanaovyo wajibika katika kumlinda mtoto dhidi ya ukatili anapokuwa katika mazingira ya shule.
Mratibu Mkuu wa kituo cha shule ya awali Bi Magreth Pataleo Mushi ameeleza mbinu wanazozitumia katika kuwapa elim bora.
Nao baadhi ya wazazi wameipongeza shule hiyo kwakuwa na walim Bora na mahari katika kuwafundisha watoto wao