Joy FM
Joy FM
28 November 2025, 15:31

Wakati tukiwa ndani ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na elimu ikiendelea kutolewa katika maeneo mbalimbali na makundi mbalimbali hasa watoto na wanawake, serikali imetakiwa kuweka sheria kali dhidi ya watuhusu wa matukio ya ukatili
Na Sadick Kibwana
Baadhi ya Viongozi wa dini Manispaa ya Kigoma Ujiji wameiomba Serikali kuboresha sheria za ukatili hasa ukatili wa kimtandao kwani umekuwa ukishamiri kwa kiwango kikubwa katika jamii ili kupunguza athari zake.
Wakizungumza katika semina iliyoandaliwa na Shirika la Womens Promotion Centre WPC chini ya mradi wa Afya yangu Uzazi wangu, Katikista wa Parokia ya Katubuka Christapio Matias Mtemwa amesema serikali ina njia nyingi ya kuzuia ukatili kwa kuelimisha jamii ama kuwakamata wahalifu hao.

Naye Mratibu wa shirika hilo ambaye ni mwezeshaji katika semina hiyo Bi Zabibu Saidi Ibrahim amesema kutolewa kwa elimu mara kwa mara imekuwa msaada wa kuwakumbusha wanajamii kuhusu athari za ukatili.
Baadhi ya Vijana katika semina hiyo wamesema zipo athari nyingi ambazo mtu anaweza kukutana nazo ikiwemo kujiua na kuathirika kisaikolojia.

Ukatili wa kijinsia ni kitendo anachofanyiwa mtu yeyote awe mwanamke au mwanaume kwa lengo la kumdhuru au kumuumiza kisaikolojia, kimwili, kiafya, kingono na kiuchumi. Hata hivyo tafiti nyingi zimeonyesha kwamba wanawake na watoto ndiyo wahanga wakuu wa ukatili wa kijinsia.