Joy FM
Joy FM
25 November 2025, 11:00

Wito umetolewa kwa wazazi na walezi wilayani Kigoma mkoani Kigoma kuwekeza kwenye elimu kwa kuhakikisha wanawasomesha watoto wao ili waweze kufikia ndoto zao.
Na Sofia Cosmas
Wazazi na walezi wametakiwa kuwapeleka watoto kusoma elimu ya awali katika shule zilizopo karibu na makazi yao ili kuepusha usumbufu wa watoto kutembea umbali mrefu kwenda shule.
Wito huo umetolewa na Mwalimu Method Pastory Kokoye kwa niaba ya Mkurugenzi wa shule ya msingi na awali ya Ndameze wakati wa mahafali ya pili katika shule ya awali ya PLATONIC DAY CARE iliyopo eneo la Kazegunga.
Amesema elimu ya awali ndio msingi mkubwa kwa watoto na hivyo wazazi hawana budi ya kuhakikisha watoto wanapata elimu ya awali.

Awali katika risala ya shule hiyo iliyosomwa na Mwalimu Belishada Masamaki ameeleza moja ya mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kukamilika kwa usajili kituo hicho ambacho kwa sasa kitaitwa PLATONIC BLILIANT ACADEMY.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Shule ya Platonic day care Mwalimu Elirehema Simon amewaomba wazazi na walezi kuweka imani yao kwenye kituo hicho kwani ni kituo kinachotoa malezi bora kwa watoto.
Nao baadhi ya wazazi wa wahitimu wamepongeza juhudi za walimu wa kituo hicho kwa kuwapa watoto malezi bora.
Shule ya Platonic day care ilianzishwa 18 Februari 2024 kikiwa na watoto 5 mpaka sasa kina watoto 70 na watoto walio hitimu ni watoto 20 .