Joy FM
Joy FM
24 November 2025, 14:34

Wakristo wameaswa kufanya kazi kwa bidii na kuacha utegemezi
Na Prisca Kizeba
Waumi wa Dini ya Kikristo Katika Manispa ya Kigoma Ujiji wameaswa kufanya kazi ili waweze kuepukana na utegemezi na kujiletea maendeleo yao binafsi na kanisa kwa ujumla.
Hayo yameelezwa na Askofu Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Western Tanganyika Emmanuel Bwata wakati wa ufunguzi wa kanisi Mtakatifu Yohana Anglikani lililopo Bagwe ambapo ameomba waumini kucha kuwa tegememezi na wajikite katika kfanya kazi.
Aidha Askofu Bwata amekemea baadhi ya viongozi wanotumia madalaka yao vibaya.
Naye Mkurugenzi wa Kanisa la Anglikana kanda ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, Andasoni Bilasa amesema kuwa kila mshiriki anao wajibu wa kujibidisha katika kufanya kazi ili kuleta maendeleo ya kanisa.
Naye Mchungaji Nadhanael Amoni wa Kanisa hilo ameeleza namna waumini walivyojikita kupambana katika kukamilisha ujenzi wa kanisa hilo liliogharim takribani shilingi milioni mia moja na arobaini na sita za kitanzania.

Baadhi ya waumini wamesema kuwa katika kutimiza mlengo ya ujenzi wakanisa kumekuwa na changamoto mbalimbali licha ya kuwa limekamilika.