Joy FM
Joy FM
20 November 2025, 15:43

Serikali ya Mkoa wa Kigoma imesema inaendelea kuthamini mchango wa mashirika mbalimbali yanayounga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya elimu
Na Lucas Hoha
Shirika la Maendeleo la Ubelgiji ENABEL limekabidhi vifaa vya kidijitali vya kufundishia shuleni kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ikiwemo komputa na sola vyenye thamani ya zaidi shilingi milioni 81 ili kuwepo na mazingira rafiki ya kujifunzia.
Elimu ni msingi wa maendeleo ya jamii na uchumi wa taifa lolote na ili mfumo wa elimu uwe bora na wenye tija, unahitaji uwekezaji mkubwa katika rasilimali watu, miundombinu, na teknolojia.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma BaloziĀ Simon Sirro ambaye anaeleza vifaa hivyo vitasaidia Mkoa kutekeleza malengo ya serikali ya kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.
Amesem kuna kila sababu za dhati kwa wakurugenzi wa Halmashauri kuvitunza vifaa hivyo ili visaidie kuzalisha wataalamu watakaokuwa na uwezo wa kushindana kwenye soko la ajira ndani na nje ya nchi.
Naye Katibu tawala wa Mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa amesema uwepo wa mashirika mbalimbali katika mkoa wa Kigoma yanayosaidia katika upande wa elimu imesaidia wanafunzi kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa hasa katika masomo ya sayansi.

Awali akikabidhi vifaa hivyo, Mtaalamu wa Elimu ya Kidijitali kutoka Enabel Bi. Lotte Van Preat amesema shirika hilo limekuwa likishirikiana na serikali katika masuala mbalimbali kupitia mradi wa wezesha binti lengo likiwa ni kuongeza uwezo wa walimu na wafunzi katika sekta ya elimu.
Katika nchi nyingi zinazoendelea, serikali pekee haiwezi kukidhi mahitaji na ndipo mashirika ya maendeleo huingia na kutoa mchango mkubwa unaolenga kuinua viwango vya elimu na kuhakikisha upatikanaji wa elimu kwa wote