Joy FM
Joy FM
18 November 2025, 13:04

Vitendo vya ukatili kwa vijana ni tabia au matendo yanayowadhuru kimwili, kihisia, kijinsia, au kijamii na ukatili huu unaweza kufanywa na watu wazima, wenzao, au hata mamlaka.
Na Sadick Kibwana
Vijana katika Manispaa ya Kigoma Ujiji wameiomba Serikali kuendelea kutoa elimu na kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto ili vitendo hivyo viweze kupungua nchini.

Wakizungumza na kituo hiki katika tamasha la burudani na elimu lililofanyika eneo la taasisi ya Kigoma Vijana Development Alliance KIVIDEA, Vijana hao wamesema kwa sasa ni muhimu elimu kutolewa zaidi kuliko kuweka nguvu katika ukamataji wa waharifu.
Mwakilishi wa Vijana katika tamasha hilo kutoka shirika la KIVIDEA Leilah Yusuf ameleza umuhimu wa tamasha hilo kwa vijana kwa elimu waliyopata.

Kwa upande wake, Mratibu kutoka KIVIDEA Nurdin Amani amesema umuhimu wa tamasha hilo ni kufikisha elimu kwa vijana ili waweze kutambua namna ya kukabiliana na vitendo hivyo.
Ikiwa ni wiki ya kuchukua hatua ambayo inafanyika kila mwaka mwezi novemba, Shirika la Kigoma Vijana Development Alliance KIVIDEA chini ya mradi wa Afya yangu Maendeleo yangu limefanya tamasha la elimu kuhusu ukatili wa kijinsia kwa kuhusisha makundi mbalimbali ya vijana.