Joy FM
Joy FM
17 November 2025, 13:20

Na Timotheo Leonard
Wananachi Mkoani Kigoma wameaswa kuzingatia lishe bora ya makundi sita ya vyakula ili kuimarisha afya zao kwa kuongeza virutubishi mwilini vinavyoimarisha mwili na akili.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa lishe Mkoa wa Kigoma James Mbalabo wakati akizungumza na Radio Joy fm kupitia kipindi cha Goodmorning Kigoma , na kusema lishe ni muhimu kwa afya ya mwanadamu.
Amesema mara nyingi magonjwa yasiyo ambukiza hutokea kutokana na na mtindo usiofaa wa vyakula na kwamba ni vyema kuzingatia matumizi sahihi ya vyakula kuepuka magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo moyo na kisukari.