Joy FM
Joy FM
17 November 2025, 12:45

Serikali Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma imesema inaendelea kuboresha miundombinu ya maji ili kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa wananchi umaimarika zaidi kwa kupata maji safi na salama
Na Sadick Kibwana
Wananchi Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma wametakiwa kusaidia kutunza na kuchangia huduma ya maji ili kusaidia upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA Wilaya ya Uvinza Mhandisi, Soud Juma Dibwine amesema hayo wakati ziara ya ukaguzi wa miradi ya maji inayotekelzwa wilayani humo.

Mhandisi Dibwine amesema kumekuwa na malalamiko ya mara kwa mara ya kukosekana kwa maji safi na salama kutokakana na uharibifu wa miundombinu ya maji unaofanywa na wananchi wasiokuwa na ustaarabu.
Mhandisi Soud Dibwine amesema wananchi wanafursa ya kuunganisha maji kwenye majumba yao kutoka kwenye chanzo kikuu.

Baadhi ya Wananchi wa Wilaya hiyo wameipongeza serikali kwa kuimarisha miundombinu hiyo.
Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Uvinza kwa kushirikiana na Shirika la Water Mission imejenga miradi ya maji yenye thamani ya zaidi ya shilingi Billion 2.5 katika vijiji vya Basanza, Msebei, Mwanganza na Mtego wa Noti ukihudumia zaidi ya wananchi elfu moja.