Joy FM
Joy FM
13 November 2025, 09:04

Serikali imetaka miundombinu ya barabara kuelekea hifadhi ya mahale kuimarishwa ili kurahsisha usafir wa watali
Na Mwandishi wetu
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro, amewaelekeza Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza, pamoja na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini TARURA, kuimarisha miundombinu ya barabara ya kutoka njia panda ya kijiji cha Rukoma kwenda Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale wilayani Uvinza yenye urefu wa kilomita 38 ili kurahisisha shughuli za utalii ndani ya hifadhi hiyo.
Balozi Sirro ametoa maelekezo hayo, baada ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale, kwa lengo la kujionea shughuli za utalii pamoja na kukutana na wawekezaji ndani ya hifadhi hiyo.

Hatua hiyo ni baada ya kuelezwa kuwa ubovu wa barabara hiyo unachangia pakubwa kuzorotesha shughuli za utalii, kwani watalii hulazimika kutumia kati ya saa tano hadi sita kufika katika Hifadhi ya Milima ya Mahale kwa njia ya barabara kutoka Kigoma Mjini.
Kwa upande wake Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale, Kamishina Msaidizi wa Uhifadhi Khalid Jumanne Mngofi, amesema kwa sasa hifadhi hiyo inafikika kwa njia ya anga na majini, lakini kwa kuimarisha miundombinu ya barabara kutaongeza idadi ya watalii na hapa anaeleza mikakati iliyopo.
Aidha ubovu wa barabara hiyo siyo tu unaathiri shughuli za utalii bali hata wananchi wa maeneo hayo nao wameeleza kuguswa pia na kero barabara hiyo.
