Joy FM
Joy FM
6 November 2025, 13:56

Serikali imeendelea kuwanoa waratibu wa Jumuiya za Kujifunza ili waweze kusiamamia maadili ya kazi
Na Emmanuel Kamangu
Waratibu wa Jumuiya za Kujifunza (JZK) katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu wametakiwa kuacha tabia ya kutanguliza posho mbele hasa wanaposhiriki mafunzo badala yake wazingatie maudhui yanayofundishwa ili kuleta matokeo chanya katika sekta ya elimu.
Wito huo umetolewa na Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Bi Elestina Chanafi, wakati akifungua mafunzo ya uongozi kwa wasimamizi wa ufundishaji na ujifunzaji ambapo amebainisha kuwa mafunzo hayo yatasaidia washiriki kuwajengea uwezo wa kutengeneza dira na kusimamia maadili ya kazi, jambo litakaloboreshwa zaidi ubora wa ufundishaji na ujifunzaji katika shule za msingi.
Kwa upande wake, Mwezeshaji wa Mafunzo Bw, Jacob Chaudo, amesisitiza umuhimu wa kufanya maamuzi yanayotegemea takwimu kuliko hisia ili kubaini tatizo la kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi wa kike na upimaji wa mwenendo wa wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Afisa Elimu taluma Msingi Bw. Joseph Maiga, amesema anamatumaini washiriki watatumia ujuzi huo kuwajengea uwezo walimu wengine katika maeneo yao ya kazi ili kufanikisha azima ya kuwa na ufaulu mzuri kwa wanafunzi.
Mafunzo haya yanayofadhiliwa na mradi wa shule bora yamehusisha wadau mbali mbali wa elimu wakiwemo wakuu wa shule na yamepangwa kufanyika kwa takribani siku nne ili kutoa fursa kwa washiriki kupata ujuzi wa kutosha juu ya namna ya kukuza taaluma shuleni.