Joy FM

DC Kasulu ataka wananchi kuendelea na shughuli zao

5 November 2025, 15:55

Mkuu wa wilaya hiyo Kanali Isaac Mwakisu, Picha na Hagai Ruyagila

Mkuu wa Wilaya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu amewataka wananchi kuendelea na shughuli zao kwa amani na utulivu

Na Hagai Ruyagila

Wananchi wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kuendelea na shughuli za uzalishaji kwa uhuru na Amani Kutokana na kuimarishwa kwa Hali ya Ulinzi na usalama katika wilayani hiyo.

Akizungumza na Vyombo vya Habari Wilayani Kasulu, Mkuu wa wilaya hiyo Kanali Isaac Mwakisu amesema kwa kushirikiana na wananchi wameendelea kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama inaimarika katika maeneo yote ya wilaya hiyo na kuhakikisha wananchi wanafanya shughuli zao kwa amani na utulivu.

Amesema wananchi wanatakiwa kuendelea kutoa ushirikiano kwenye vyombo vya ulinzi na usalama wanapobaini viashiria vya uvunjifu wa amani ili viweze kudhibitiwa na kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani.

Sauti ya Mkuu wa wilaya hiyo Kanali Isaac Mwakisu

Aidha Kanali Mwakisu ameongeza kuwa Maeneo ya mipakani yameendelea kuimarika katika hali ya usalama kuhakikisha wananchi wanafanya shughuli mbalimbali na kutoa huduma bora katika familia kwa kuzingatia usalama wao na mali zao.

Sauti ya Mkuu wa wilaya hiyo Kanali Isaac Mwakisu

Kwa upande wao, baadhi ya wananchi wilayani Kasulu wamesema kila mmoja anatakiwa kutambua umuhimu wa kudumisha amani kwa kushirikiana na jeshi la Polisi kufichua vitendo vya uhalifu na wahalifu ili jamii iweze kufanya shughuli kwa hali ya amani kwa ajili ya ustawi wa wananchi.

Sauti ya wananchi wa kasulu