Joy FM
Joy FM
27 October 2025, 12:42

Serikali imeendelea kuhamasisha wananchi kuzingatia suala usafi wa mazingira kama ambavyo sheria ya mazingira ya 2016 inavyoelekeza kila mwananchi kuhakikisha mazingira yanayomzunguka yanakuwa safi salama
Na Hagai Ruyagila
Wananchi katika Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kuhakikisha wanadumisha usafi wa mazingira katika maeneo yao ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa Kipindupindu.
Wito huo umetolewa na Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu, Bw Ibrahimu Mwangarume wakati wa maadhimisho ya usafi wa mazingira yaliyofanyika katika soko kuu la Kumsenga Halmashauri ya Mji Kasulu.
Bw. Mwangarume amesema kuwa usafi wa mazingira ni jambo la msingi katika maisha ya mwanadamu, hivyo ni wajibu wa kila mfanyabiashara na mkazi kuhakikisha mazingira yanakuwa safi wakati wote.

Kwa upande wake, Afisa Afya Mazingira na Mkuu wa kitengo cha Usafi na udhibiti taka Halmashauri ya Mji Kasulu Bw. Msafiri Nkimbili amezungumzia sababu ya ushiriki mdogo wa wananchi katika siku ya usafi lakini amesema tayari Halmashauri imebaini mwarobaina wa changamoto hiyo.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Kumsenga Bi. Rozina Mengo amesema wamaeneo yao yameendelea kuwa safi kutokana na kutoa hamasa kwa wananchi kushiriki katika shughuli za usafi wa jamii ili kukuepuka magonjwa ya mlipuko.
Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Kasulu wamesema usafi wa mazingira ni wamuhimu kwa kila kaya lakini wamekuwa wakishindwa kushiriki zoezi hilo la usafi kutokana na kukosa hamasa na elimukutoka kwa viongozi wao.