Joy FM

Wanafunzi walia na wazazi kuwachagulia masomo Kigoma

6 October 2025, 10:03

Wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Mikamba, Picha na Emmanuel Kamangu

Wito umetolewa kwa wazazi na walezi kuwaunga mkono watoto wao katika masomo wanayopenda kusoma na kuacha kuwalazimisha kusoma masomo ambayo hawayawezi

Na Emmanuel Kamangu

Wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Mikamba Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma wamewaomba wazazi kuacha tabia ya kuwachagulia masomo ya kusoma kwani kufanya hivyo ni kukatiza ndoto zao.

Wamebainisha hayo wakati wa mahafali yao ya kuhitimu kidato cha nne shule ya sekondri Mikamba ambapo wamesema kumekuwa na changamoto ya wazazi waliowengi kuwataka wasome masomo ya sayansi pekee jambo ambalo limekuwa likisabisha baadhin yao kuwa na ufaulu mdogo.

Aidha mgeni rasmi katika mahafari hayo ambaye ni Kaimu Meneja Biashara kutoka Benki ya CRDB Mkoani Kigoma Bw. Gervas Makomola ameeleza kuwa swala la wazazi kuwalazimisha watoto wao kusoma masomo ya sayansi ni kuwanyima uhuru wa kuchagua mchepuo wanaoupenda kwa malengo yao ya baadaye.

Mgeni rasmi ambaye Kaimu Meneja wa biashara Benki ya CRDB, Bw. Gervas Makomola akiwa katika mahafali ya kidato cha nne shule ya sekondari Mikamba

Kwa upande wake, Mkuu wa shule ya sekondari Mikamba Bw. James Kivula amewaomba wazazi kuheshimu wanachokichagua kusoma watoto wao kwani kila masomo yana umuhimu wake huku Meneja wa shule hiyo Bw. Ezra Mikamba akiwaomba wazazi kulipa ada kwa wakati ili kuharakisha shuguli za maendeleo ya wanafunzi na shule kwa ujumla.

Meneja wa shule ya sekondari Mikamba Ezra Mikamba akizungumza wakati wa mahafali ya kidato cha nne, Picha na Emmanuel Kamangua

Hata hivyo, baadhi ya wazazi na walezi wa wahitimu wamesema wana wajibu wakitimiza jukumu la malezi kwa watoto wao huku wakiahidi kushirikiana vizuri na uongozi wa shule ili watoto wao waendelee kufanya vizuri katika masomo yao