Joy FM

Zaidi ya wananchi laki 2 wapatiwa matibabu ya kibingwa nchini

2 October 2025, 08:39

Katibu tawala Mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa akiwa kwenye picha na madaktari bingwa waliowasili Kigoma kutoa huduma za matibabu, Picha na Tryphone Odace

Wananchi zaidi ya elfu saba mkaoni Kigoma wamenufaika na huduma ya matibabu kutoka kwa madaktari bingwa wabobevu wa Mama Samia na kuokoa maisha ya Watanzania hasa wenye hali ya chini.

Na Tryphone Odace

Wananchi zaidi ya laki mbili wamepatiwa matibabu ya kibingwa na bingwa bobezi kote nchini kupitia kambi ya madaktari bingwa wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, huku watoa huduma laki moja wakijengewa uwezo wa kutoa huduma tangu kuanza kwa mpango huo mwezi Mei mwaka 2024.

Hayo yameelezwa na Grace Maliki kutoka Wizara ya Afya Idara ya Afya Uzazi Mama na Mtoto, wakati wa mapokezi ya Madaktari Bingwa 48 kutoka hospitali mbali nchini, watakaotoa huduma za matibabu ya kibingwa katika halmashauri zote nane za mkoa wa Kigoma katika muda wa juma moja kuanzia leo Jumatatu Septemba 29, 2025.

Sauti ya Grace Maliki kutoka Wizara ya Afya Idara ya Afya
Katibu tawala Mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa akiwa kwenye picha na madaktari bingwa waliowasili Kigoma kutoa huduma za matibabu, Picha na Tryphone Odace

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa, amesema hatua hiyo ni muhimu ikizingatiwa kuwa bado kuna changamoto ya ukosefu wa huduma bobezi hasa kwa mikoa ya pembezoni ikiwemo mkoa wa Kigoma.

Sauti ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt. Damas Kayera, amesema ujio wa madakatari bingwa hao utaboresha utoaji wa huduma katika mkoa wa Kigoma, kwa watumishi kupata mafunzo na kuwa na uelewa zaidi wa kutoa hizo kwa siku zijazo.

Sauti ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt. Damas Kayera