Joy FM
Joy FM
26 September 2025, 17:30

Mfuko wa hifadhi ya jamii wa NSSF umegawa mitungi ya gesi kwa mam lishe, baba lishe na wastaafu ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jududi za serikali katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Na Tryphone Odace
Mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro amesema Mfuko wa Hifadhi ya jamii kwa watumishi wa Umma (NSSF) umeendelea kuboresha maisha ya watanzaia hivyo ameomba uungwe mkono ili kuhakikisha utekelezaji wake wa majukumu haukwami.
Balozi Sirro alisema hayo akikabidhi mitungi 200 ya gesi ya kupikia kwa wajasiriamali na wastaafu ambao ni wanachama wa NSSF katika Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Mkuu huyo wa mkoa Kigoma alisema kuwa, mkoa una fursa za utalii na biashara hivyo kuuomba uongozi wa Taasisi hiyo kuwafikia watu wengi zaidi na kuwasajili kuwa wanachama ili waweze kupata fursa mbalimbali za mafao zinazotolewa na mfuko huo.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa mkoa Kigoma kukabidhi mitungi hiyo ya gesi, alisema kuwa inafahamika mkoa umechaguliwa kuwa eneo la kimkakati kiuchumi na biashara hivyo NSSF imeona itoe mitungi hiyo kwa wanachama wao ili kuunga mkono shughuli zao za biashara hususani katika kuimarisha shughuli zao maarufu kama Staa wa mchezo.
Mshomba alisema kuwa NSSF imeazimia kuwafikia watu wote walioajiairi kuhakikisha wanajiunga na mfuko huo ili kuweza kuweka akiba, kupata mafao na mikopo mbalimbali, ikiwa na maagizo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.