Joy FM

Umuhimu wa uzazi wa mpango, ushiriki wa wanaume Kigoma

26 September 2025, 14:59

Akina mama na akina baba wakiwa katika sehemu yautoaji wa huduma za afya ya uzazi kwa mama na mtoto, Picha na TryphoneOdace

Uzazi wa mpango ni moja ya nyenzo muhimu katika kuimarisha afya ya jamii, kukuza ustawi wa familia na kuchochea maendeleo kiuchumi.

Huu ni mchakato unaowezesha wanandoa au watu binafsi kupanga idadi ya watoto wanaotaka kuwapata, muda wa kuwapata na nafasi kati ya mtoto mmoja na mwingine kwa kutumia njia salama na sahihi. Ingawa kwa muda mrefu suala hili limechukuliwa kama jukumu la wanawake pekee, mchango wa wanaume ni wa msingi katika kuhakikisha mafanikio ya mpango huu.