Joy FM
Joy FM
25 September 2025, 15:46

Serikali imesema itaendelea kuweka mikakakti ya kuwawezesha wanafaika wa mikopo ya asilimia kumi ili waweze kujiinua kiuchumi
Na Sadick Kibwana
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dkt Rashid Chuachua, ametoa wito kwa wananchi zaidi ya 500 ambao ni wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 kwa Vikundi 58, kutotumia mikopo hiyo kama zawadi na kufanya mambo kinyume na lengo la mikopo hiyo inayotolewa na Serikali.
Dk. Chuachua ametoa kauli hiyo katika Ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 walio ndani ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, ambapo amesema ni vyema kwa kikundi chochote ambacho kitanufaika kukumbuke kurejesha ili kuwezesha wengine kupata katika awamu inayofuata ya utoaji wa mikopo hiyo.
Naye Jabir Majira ambaye ni Afisa wa Maendeleo Manispaa ya Kigoma Ujiji, amewaomba wanufaika kutumia mafunzo hayo kama msingi imara wa kuwasaidia kibiashara pindi wapatapo mikopo hiyo.
Baadhi ya wanufaika na Mikopo hiyo wameishukuru Serikali na kuahidi kuitumia kama ilivyokusudiwa.

Mikopo ya asilimia 10 ya serikali inatolewa kwa kushirikiana na Benki ya CRDB ambapo kwa awamu hii zaidi ya shilingi milioni 555 zinatolewa kwa vikundi 58 ambavyo vitanufaika na mpango huu ikiwa ni awamu ya pili toka mwaka 2023 baada ya kusitishwa.