Joy FM

Mwenge wa uhuru wazindua kituo cha sayansi Buhigwe

22 September 2025, 14:03

Wanafunzi wakiendelea kujifunza tehama kwa vitendo, Picha na EmmanuelKamangu

Jumla ya miradi 7 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 2 wilayani Buhigwe Mkoani Kigoma imetembelewa,kuzinduliwa na mingine kuwekewa mawe ya msingi na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa Ismail Ali Ussi.

Na Emmanuel Kamangu

Mwenge wa uhuru umezindua kituo cha sayansi wilayani Buhigwe mradi unaoenda kuwasaidia wanafunzi na watu mbali mbali kujifunza tecnolojia kwa vitendo.

Akizungumza wakati akizindua mradi huo kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Bw,ismail Ali ussi amesema kituo hicho ni fursa kwa vijana wengi pamoja na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kujifunza sayansi kwa vitendo.

Awali meneja wa mradi wa kituo hicho cha sayansi  Bw, Maximilian singu akisoma tarifa ya mradi mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge amesmea mradi  huo ambao umejengwa kwa ufadhili wa serikali ya Canada kupitia shirika la UNICEF Umegalimu million 260 huku akibainisha kuwa lengo la stem hiyo ni kuhakikisha wanafunzi wanapenda masomo ya sayansi.

Kiongozi wa mbio za mwenge akizungumza na Meneja wa mradi wa kituo cha sayansi Buhigwe wakati akikagua mradi huo, Picha na Emmanuel Kamangu

Aidha wanafunzi kutoka shule mbali mbali wilayni Buhigwe ambao wamefika eneo la kituo hicho kujifunza sayansi kwa vitendo wamesema kituo hicho kitawasaidia kwa kiasi kikubwa kupenda masomo ya sayansi tofauti na awali ambapo walisoma masomo  hayo kwa nadharia.

Hata hivyo wanafunzi hao wameishukuru serikali kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya elimu hasa kwa kuhakikisha mtoto hatembei umbali mrefu kufuata  eilimu.

Sauti ya mwandishi wetu Emmanuel Kamangu