Joy FM
Joy FM
18 September 2025, 15:30

Wananchi wa Kata ya Kagera Manispa ya Kigoma Ujiji, wameomba mgombea ubunge wa jimbola Kigoma mjini Zitto Kabwe kuwasiadia kutatua changamoto ya uwepo mikopo umiza.
Na Mwandishi wetu
Mgombea ubunge jimbo la Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameahidi kukomesha mikopo yenye riba kubwa maarufu kausha damu kwa wananchi endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo, kwa kuanzisha mfuko maalum ambao ataweka shilingi bilioni 1 ili wananchi waweze kukopa bila riba.
Zitto amesema hayo wakati wa kampeni zake za kuwania nafasi ya ubunge katika Jimbo la Kigoma Mjini zilizofanyika katika kata ya Kagera Manispaa ya Kigoma Ujiji, Septemba 17, 2025.

Amesema wananchi wamekuwa wakishindwa kuendelea kutokana na mikopo umiza hali inayosababisha washinde kuendelea kimaisha.