Joy FM
Joy FM
16 September 2025, 09:56

Mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka 2025 zimeanza rasmi mkoani Kigoma ambapo miradi 16 ikitarajiwa kuwekewa mawe ya Msingi, mmoja kufunguliwa, 27 kuzinduliwa huku mingine 12 ikitembelewa na kukaguliwa.
Na Tryphone Odace
Mwenge wa uhuru umeanza mbio zake Mkoani Kigoma ambapo utapitia miradi 56 yenye thamani ya shilingi Bilioni 64.7 ambapo ukiwa mkoani humo mwenge huo wa uhuru utatembea kilimotea 777.1 katika halmashauri nane za mkoa Kigoma.
Mkuu wa Mkoa Kigoma, Balozi Simon Sirro amesema hayo wakati akipokea mwenge wa uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa Kagera Fatuma Mwassa katika makabidhiano yaliyofanyika katika kijiji cha Nyakibuye Wilaya Kakonko Mkoani Kigoma.
Balozi Sirrtio alisema kuwa katika miradi itakayopitiwa na mwenge miradi 16 itawekewa mawe ya msingi, mmoja utafunguliwa, miradi 27 kuzinduliwa na miradi 12 itatembelewa.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa katika miradi inayotembelea na mwenge Wananchi wamechangia kiasi cha shilingi milioni 283, halmashauri shilingi bilioni 1.6, wahisani shiliingi Bilioni 53 na serikali kuu ni bilioni 6.6.

Katika siku ya kwanza ya mbio zake mkoani Kigoka Mwenge wa uhuru ulikimbizwa katika wilaya ya Kakonko ambapo Mkuu wa wilaya hiyo Evance Malasa amesema kuwa ukiwa Wilayani humo mwenge huo wa uhuru utatembelea miradi saba yenye thamani ya shilingi bilioni 2.2 ukikimbizwa kwa umbali wa kilometa 135.