Joy FM

Miradi 7 kutembelewa na mwenge wa uhuru Buhigwe

11 September 2025, 14:17

Mratibu wa mwenge wa uhuru wilayani Buhigwe Bw, Mathias  Lema, Picha na Emmanuel Kamangu

Wananchi Wilayani Buhigwe Mkoani Kigoma wametakiwa kujitokeza kuupokea mwenge wa uhuru ambao unatarajiwa kuingia Wilayani humo September 19

Na Emmanuel Kamangu

Mwenge wa uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma unatarajia  kutembelea  miradi saba ya maendeleo.

Mratibu wa Mwenge wa Uhuru Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Bw. Mathias Lema ameitaja miradi itakayozinduliwa kuwa  ni mradi wa  maji, mradi wa vyumba vinne vya vya madarasa, mradi wa vijana wajasiriamali kukopeshwa guta tatu na piki piki mbili, mradi wa zahanati ya Lemba, mradi wa kituo cha sayansi, huku mradi mmoja wa barabara ukiwekewa jiwe la msingi na mradi wa shamba la miti ukitembelewa.

Amesema kuwa miradi yote hiyo imeghrimu zaidi ya shilingi billion 2.

Sauti ya Mratibu wa mwenge wa uhuru Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Bw. Mathias Lema

Aidha Bw. Lema amewataka wananchi wilayani humo kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kupokea mwingi wa uhuru ambao unafika kwao kuangaza miradi mbali mbali ya maendeleo.

Sauti ya Mratibu wa mwenge wa uhuru Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Bw. Mathias Lema

Kwa upande wao, Baadhi ya wananchi wamesema mwenge wa uhuru ni Tunu kwao kutokana na kuendelea kuangaza maendeleo yao uhuru wao na umoja wao kama watanzania.

Sauti za wananchi

Mwenge wa uhuru kwa Wilaya ya Buhigwe utawasili September 19 mwaka huu na kukimbizwa kwa siku mbili kwa ajili ya kutembelea miradi ya maendeleo Wilayani humo.