Joy FM
Joy FM
8 September 2025, 14:43

Wito umetolewa kwa waganga wa jadi kuacha kupiga ramli chonganishi kwenye jamii kwani zimekuwa zikileta uchonganishi kwa wananchi na kuchochea migogoro
Na Sofia Cosmas
Wakristo katika Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma wametakiwa kuachana na imani za kishirikina na badala yake kumrudia Mungu kwani imani hiyo zimekuwa zikichochea migogoro kwenye jamii.
Hayo yameelezwa na Mchungaji wa kanisa la AGGCI Malagarasi lililop Wilayani Uvinza Mch Meshack John ambapo amewataka waamini wa dini ya kikristo na wasio wakristo kuachana na imani za kishirikina kwani imani hizo hupelekea athari kwa wananchi kama upotevu wa nguvu kazi kwa taifa.
Naye Mwenyekiti wa kijiji cha malagarasi akiwakilishwa na Acley Wiliamu amempongeza Mchungaji wa kanisa hilo kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuombea jamii na kuokoa maisha ya watu katika kijiji hicho.
Baadhi ya waumini akiwemo Hashimu Ally ambaye alikua ni moja ya waganga wa kienyeji ambao walikua wanajihusisha na imani za kishirikina wamewashauri watu kuachana imani hizo na kumrudia Mungu kwani hakuna faida katika imani hizo mbali na uchonganishi kwa jamii.