Joy FM
Joy FM
29 August 2025, 17:30

Wafanyabiashara wadogowadogo Mkoani Kigoma wametakiwa wametakiwa kuchangamkia fursa za mikopo inayotolewa na taasisi za benki na Halmashauri ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Na Orida Sayon
Shirikisho la umoja wa machinga Tanzania (SHIUMA) kanda ya magharibi limefanya kongamano la kumpongeza Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa uboreshaji wa miundombinu ya biashara.
Kongamano hilo limefinyika leo katika uwanja wa katubuka sekondari manispaa ya kigoma ujiji ikihusisha mikoa ya Katavi, Kigoma,Tabora na Rukwa
Akitoa taarifa ya hali ya usajili wa wafanyabiashara ndogondogo, Afisa biashara Baraka Fubusa amesema jumla ya wafanyabiashara 4026 wamesajiliwa katika mfumo wa wanyabiashara ndogondogo mkoani Kigoma.

Aidha ameeleza kuwa wafanyabiashara wengi wamekuwa na madeni mengi katika taasisi za kifedha, na kukosa mwitikio wa kulipia vitambulisho vya wafanya biashara ndogondogo hali inayopelekea kukosa mikopo ili kujikwamua katika biashara zao.
Licha ya uwepo wa mafanikio na uboreshwaji wa miundombinu ya biashara ukosefu wa elimu ya mikopo na kukosa mitaja ni miongoni mwa changamoto zinazowakumba wafanyabiashara.
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dkt Rashid Chuachua akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kigoma katika kongamano hilo amewataka wafanyabiashara hao kuchangamkia fursa ya mikopo inayotolewa na taasisi za kifedha na mikopo inayotolewa na halmashauri ili kujikwamua kiuchumi.
