Joy FM

Mwarobaini ukatili kwa wanawake na watoto wapatikana Kigoma

28 August 2025, 15:49

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr Rashid Chuachua akiwa katika hafla ya kupokea na kukabidhi pikipiki 15, Picha na Ofisi ya Mkoa

Serikali imesema itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kukabiliana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto.

Na Josephine Kiravu

Wadau wa maendeleo Mkoani Kigoma wametakiwa kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kukabiliana na changamoto ya uwepo wa matukio ya ukatili kwa wanawake na watoto huku maafisa wawezeshaji wanawake kiuchumi wakitakiwa pia kuhakikisha asilimia 30 inayotengwa kwa ajili ya wanawake inatumika ipasavyo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr Rashid Chuachua kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma katika hafla ya kupokea na kukabidhi pikipiki 15 kwa maafisa wawezeshaji wanawake kiuchumi kutoka halmashauri zote pamoja na jeshi la polisi kitengo cha dawati la jinsia na watoto.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr Rashid Chuachua
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr Rashid Chuachua akiwa katika hafla ya kupokea na kukabidhi pikipiki 15, Picha na Ofisi ya Mkoa

Kwa upande wake, Katibu Tawala mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa amewataka maafisa wote waliokabidhiwa pikipiki hizo kuzitumia vyema kwa kuhakikisha wanafika maeneo yote kwa wakati na kupunguza vitendo vya ukatili.

Sauti ya Katibu Tawala mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa

Na hapa mwakilishi wa mkurugenzi mkazi UN Women Tanzania Ongagwa Gwambaye amesema kupitia pikipiki hizo wanaimani wanawake wengi zaidi na mabinti watafikiwa kwa wakati lengo likiwa ni kuimarisha wanawake katika maeneo tofauti ikiwemo kuwapatia elimu ya uwezeshaji kiuchumi.

Sauti ya mwakilishi wa mkurugenzi mkazi UN Women Tanzania Ongagwa Gwambaye

Nao baadhi ya maafisa waliopatiwa pikipiki hizo akiwemo Mkuu wa polisi jamii mkoa wa Kigoma ACP Wilfred Majura wamesema hapo awali walipata changamoto kufika kwa wakati kwenye matukio lakini kupitia uwezeshaji huo itasaidia kuwafikia waathirika wa ukatili kwa wakati.

Sauti ya baadhi ya maafisa waliopatiwa pikipiki hizo