Joy FM

Wamiliki shule waaswa kuendana na mabadiliko ya mtaala mpya

25 August 2025, 16:37

Mdhibiti Mkuu ubora wa shule Wilaya Kibondo Canon Mley, Epifania Yaba, Picha na Hagai Ruyagila

Mmiliki wa shule za Hekima zilizopo Mjini Kasulu Mkoani Kigoma Fedia Yaredi amesema ataendelea kusimamia shule hizo ili zieweze kutoa elimu bora kwa watoto

Na Hagai Ruyagila

Wamiliki wa shule binafsi wilayani Kasulu mkoani Kigoma wameshauriwa kukubaliana na mabadiliko ya mtaala mpya ambao umetolewa na serikali ili kuboresha sekta ya elimu nchini.

Wito huo umetolewa na Mdhibiti mkuu Ubora wa shule wa wilaya ya Kibondo Canon Mley, Epifania Yaba wakati wa mahafari ya dasara la saba na kidato cha nne katika shule za hekima zilizopo mjini Kasulu.

Canon Mley, Yaba amesema utekelezaji wa mtaala mpya unalenga kuleta mageuzi chanya katika elimu kwa kuwajengea wanafunzi ujuzi wa vitendo, fikra bunifu na uwezo wa kujitegemea hivyo amemuomba mkurugenzi wa shule hizo kuanzisha madarasa hayo ambayo yatasaidia taifa kupata wataalamu mahiri katika Nyanja mbalimbali.

Sauti ya Mdhibiti mkuu Ubora wa shule wa wilaya ya Kibondo Canon Mley, Epifania Yaba

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa shule za Hekima zilizopo wilaya ya Kasulu, Fedia Yaredi amesema mabadiliko hayo ni chachu ya kukuza vipaji na ujuzi wa kitaaluma ili wahitimu waweze kuingia katika soko la ajira.

Sauti ya Mkurugenzi wa shule za Hekima zilizopo wilaya ya Kasulu, Fedia Yaredi
Mkurugenzi wa shule za Hekima zilizopo wilaya ya Kasulu, Fedia Yaredi, Picha na Hagai Ruyagila

Baadhi ya wazazi akiwemo Richard Jonas kutoka Kabanga na Esta Martin wameunga mkono mabadiliko ya mtaala katika sekta ya elimu ambayo yatasaidia mwanafunzi atakapohitimu atakuwa na ujuzi utakaomsaidia katika maisha yake.

Sauti ya baadhi ya wazazi akiwemo Richard Jonas kutoka Kabanga na Esta Martin
Baadhi ya wazazi akiwemo Richard Jonas kutoka Kabanga na Esta Martin, Picha na Hagai Ruyagila