Joy FM
Joy FM
25 August 2025, 14:08

Wito umetolewa kwa shule binafsi kuanza kufuata mabadiliko ya mtaala mpya ambao umetolewa na serikali ili kuboresha sekta ya elimu nchini.
Na Sofia Cosmas
Watumishi wa umma na sekta binasi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji wametakiwa kuondoa utengano na chuki badala yake washikamane kuleta wazo la pamoja katika kuijenga Kigoma na Taifa la Tanzania.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Cambrige Shire Josephati Chales Njige wakati wa mahafari ya nne ya darasa la saba katika shule ya msingi na awali ya Cambrige Shire Academy ambapo amewataka watumishi wa Umma na Sekta binafsi kushirikiana kwa pamoja ili kuijenga Kigoma na taifa kwa ujumla.
Awali katika risala kwa mgeni rasmi iliyosomwa na Meneja wa shule hiyo ya Cambrige Shire Academy Mwl Lazaro Kiguja amesema mafanikio ya shule hiyo yanatokana na misingi na malengo waliyojiwekea kama anavyoeleza hapa.
Akijibu risala mgeni rasmi katika sherehe hizo, Afisa kutoka Ofisi ya Udhibiti Ubora Rusi Nyanda amewapongeza walimu wa Shule hiyo na kuahidi kubeba changamoto walizoziainisha kuzipeleka panapohusika.
Kwa upande wao, baadhi ya wazazi na wanafunzi katika shule hiyo wamewataka wazazi na walezi kuwafundisha watoto wao hasa mtaala mpya kwa vitendo.