Joy FM
Joy FM
19 August 2025, 17:33

Katika jamii yoyote ile, watoto ni nguzo muhimu ya maendeleo ya sasa na baadaye na maadili ni msingi wa malezi bora yanayomuwezesha mtoto kuwa raia mwema na mwenye mchango chanya kwa jamii hata hivyo, katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko la ukosefu wa maadili miongoni mwa watoto na kutatiza wasiwasi mkubwa kwa wazazi, walimu na jamii kwa ujumla.
Na Sadick Kibwana
Wazee wa Kimila Mkoani Kigoma wameiomba serikali kushirikiana na viongozi wa kijamii na kidini ili kusimamia maadili nchini na kusaidia taifa kuwa na kizazi salama.
Hayo yamebainishwa katika semina iliyoandaliwa na taasisi ya Women’s Promotion Center WPC, ambapo mwenyekiti wa Baraza la Mzee Jummane Fumawicha.
Mkurugenzi wa Taasisi ya WPC Martha Jerome amesema mafunzo hayo yanalenga kutoa msisitizo kwa wazazi kuvunja ukimya na kuzungumza na watoto wao kuhusu athari za ukosefu wa maadili.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria semina hiyo akiwemo Bi Bora Rajabu Juma na Himidi Magoha wamesema mmomonyoko wa maadili umesababishwa na wazazi kutotilia maanani suala la malezi.
Mmomonyoko wa Maadili umekuwa ukiongezeka duniani kote sababu ikiwa ni matumizi yasiyosahihi ya teknolojia katika jamii huku kundi kubwa linaloathirika wakiwa ni vijana.