Joy FM

Wanawake washauriwa kushiriki kwenye ngazi za maamuzi

18 August 2025, 14:46

Wanawake wa kanisa la Pentekoste moto moto tawi la Muzye, Picha na Hagai Ruyagila

Wanawake wameshauriwa kushiriki katika katika shughuli mbalimbali ikiwemo uongozi

Na Hagai Ruyagila

Wanawake wa kata ya Muzye Halmashauri ya wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kuwa na msimamo thabiti na kujitokeza kwa wingi kushiriki shughuli za maendeleo pamoja na kuchangamkia nafasi za uongozi katika jamii zao.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Idara ya wanawake kanisa la Pentekoste moto moto tawi la Muzye Bi. Gaudensia Andrea wakati wa ibada ya sherehe ya akina mama iliyofanyika kanisani hapo.

Bi. Gaudensia amesema ni muhimu wanawake kuweka mikakati madhubuti ya kujiinua na kushiriki kikamilifu katika masuala ya kijamii, kiuchumi na kisiasa badala ya kuwaachia wanaume pekee kufanya maamuzi muhimu katika jamii.

Saudi ya Mwenyekiti wa Idara ya wanawake kanisa la Pentekoste
Wanawake wa kanisa la Pentekoste moto moto tawi la Muzye, Picha na Hagai Ruyagila

Kwa upande wake, Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo, Mchungaji William Bazega amewataka wanawake kutambua nafasi yao ya kipekee sit u katika familia bali pia katika kanisa.

Sauti ya Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo, Mchungaji William Bazega

Baadhi ya wanawake walioshiriki katika ibada hiyo wameunga mkono wito huo na kueleza kuwa wamehamasika kuchukua hatua zaidi katika kujihusisha na masuala ya maendeleo.

Sauti ya Wanawake

Sherehe hiyo ya akina mama ilihuruliwa na waumini kutoka maeneo mbali mbali ya kata ya Muzye.