Joy FM
Joy FM
18 August 2025, 08:08

Kuanza kwa ujenzi wa Reli na kukamilika kwake kutasaidia kufungua fursa kwa wananchi wetu ambao wataweza kutoka Burundi hadi Dar es Salaam ndani ya siku moja pamoja na usafirishaji wa mizigo ambapo hivi sasa, lori linatumia saa 96 kutoka Dar es Salaam hadi Bujumbura lakini baada ya kukamilisha ujenzi, usafirishaji wa mizigo kwa kutumia treni utatumia saa 20 tu.
Na Tryphone Odace
Tanzania na Burundi zimeweka jiwe la msingi ili kuanza ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kutoka Wilayani Uvinza hadi Musongati nchini Burundi kwa gharama ya zaidi ya dora za marekani bilioni mbili, ikiwa ni mkakati wa kuboresha usafiri na usafirishaji kwa njia ya reli na kukuza uchumi kwa nchi hizo.
Rais wa Jamhuri ya Burundi Evariste Ndayishimiye pamoja na Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa wameongoza maelfu ya raia wa Burundi kushuhudia uwekaji jiwe la msingi kuanza ujenzi wa mradi wa reli hiyo ya SGR.

Katika hotuba ya Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, amesemaReli hiyo inaenda kufungua ukurasa mpya wa uhusiano na Tanzania na Burundi sambamba na kukuza uchumi hasa kupitia usafirishaji wa madini.
Waziri mkuu wa Tanzania Kassimu Majaliwa amesema mradi huo utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitato na kukamilika kwake utachochea kasi ya biashara kwa kuzalisha pia viwanda vingi kwa ukanda wa mgaharibi.
Hata hivyo, Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema kukamilika reli hiyo, itachagiza ongezeko la mizigo mingi inayosafirishwa na kuondoa adha kwa wafanyabiashara wanaoshidwa kusafirisha mizigo na bidhaa kwa wakati.
