Joy FM
Joy FM
13 August 2025, 15:29

Wito umetolewa kwa wazazi na walezi kuendelea kutoa taarifa na ushirikiano pindi matukio ya ukatili yanapotokea ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa.
Na Emmanuel Kamangu
Mabaraza ya watoto Wilayani Buhigwe Mkoani Kigoma yametajwa kuwa chachu ya kupungua kwa matukio ya ukatili kwa watoto.
Amebainisha hayo Afisa maendeleo ya jamii wilayani Buhigwe Bw, Christopha kajange katika kikao ambacho kimewahusisha viongozi wa Dini na baadhi ya wananchi ikiwa ni kutoa tathimini ya hali ya ukatili wilayani humo ambapo amesema kwa kasuhirikiana na shirika la kuhudumia watoto Dunia UNICEF wameendelea kujizatiti kuhakikisha mtoto anabaki salama zidi ya vitendo vya ukatili.

Kwa upande wake, Afisa ustawi wa jamii wilayani humo Bw. Agrey Mwambete amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanakuwa karibu na watoto ili kujua kila jambo wanalolipitia wakiwa nje na nyumbani.
Baadhi ya viongozi wa dini wilayani humo wamesema wataendelea kushirikiana na serikali ili kuhakikisha jamii inaondokana na vitendo vya ukatili.
Aidha Mkuu wa dawati la jinsia na watoto wilayani Buhigwe mhadhamu miyonga amewataka wazazi na walezi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi pindi wanapoona matukio ya ukatili na kuepuka kuyashugulikia kifamilia.