Joy FM
Joy FM
6 August 2025, 13:18

Akina mama wametakiwa kuhakikisha wanawanyonyesha watoto maziwa ya mama ili waweze kupata virutubisho
Na Josephine Kiravu
Imeelezwa kuwa viwango vya unyonyeshaji wa maziwa ya mama nchini Tanzania vinaendelea kuimarika, huku asilimia ya watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya mama pekee ikiongezeka kutoka asilimia 58 mwaka 2018 hadi aslimia 64 mwaka 2024.
Kwa mujibu wa Takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Katibu mkuu wa wizara ya afya Dr Seif Shekalaghe watoto wanaonyonyeshwa ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa wameongezeka kutoka asilimia 58 mwaka 2018 hadi aslimia 70 mwaka 2022.
Wataalamu wa afya wamekuwa wakisistiza akina mama kuwanyonyesha watoto wao angalau kwa kipindi cha miezi 20, hata hivyo mpaka sasa inaelezwa kuwa ni asilimia 35 tu ya watoto wenye umri wa miezi 20 hadi 24 wanaoendelea kunyonya hali inayotajwa kuhatarisha mahitaji ya lishe bora kwa watoto hao kama anayoeleza hapa Afisa lishe Manispaa ya Kigoma ujiji Mastidia Gabriel.
Lakini je ipi ni nafasi ya akina baba katika kuhakikisha mama ananyonyesha mtoto kwa kipindi cha miezi 6 ya mwanzo.
Ustadhi Maliki Ahmad ni baba ambaye amekuwa akihakikisha mwenza wake anamnyonyesha mtoto kwa kufuata muongozo wa afya pamoja na kuhakikisha anapata lishe bora huku mwenza wake akileza furaha yake kwa kupata huduma hizo.
Agosti mosi hadi 7 ya kila mwaka ilitengwa kama wiki ya unyonyeshaji kwa lengo la kuhamasisha akina mama kutambua umuhimu wa unyonyeshaji wa maziwa mama na mwaka huu maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji yanaenda na Kauli mbiu isemayo “Thamini unyonyeshaji weka mazingira wezeshi kwa mama na mtoto”