Joy FM

Viongozi wa dini watakiwa kuepuka ubaguzi Kigoma

1 August 2025, 11:43

Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro, Picha na Hagai Ruyagila

Mkuu wa Mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro amewaasa viongozi wa dini kuwa na mshikamano wa pamoja katika kuwahumia waumini na jamii kwa ujumla

Na Hagai Ruyagila

Viongozi wa umoja wa makanisa ya Kipentekoste Mkoa wa Kigoma wametakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano ili kudumisha upendo na amani katika jamii.

Viongozi hao wamekutana pamoja katika kanisa la EAGT Beloya Kasulu mjini kwa ajili ya kufanya uchaguzi wa viongozi wa umoja wa makanisa ya kipentecoste CPCT mkoa wa Kigoma baada ya waliokuwa katika uongozi huo kumaliza muda wao wa uongozi.

Viongozi wa dini wakiwa katika ufunguzi wa zoezi la uchaguzi, Picha na Hagai Ruyagila

Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa zoezi hilo la uchaguzi, Mkuu wa mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro ambaye amewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe kanali Michael Ngayalina akisoma hotuba amesema viongozi wa dini wanatakiwa kuepuka ubaguzi badala yake wadumishe upendo na amani katika jamii pamoja na kuimarisha ushirikiano na madhehebu mengine.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe kanali Michael Ngayalina

Kwa upande wake, Askofu wa Kanisa la PMC na mjumbe wa halmashauri kuu ya umoja wa makanisa ya Kipentekoste CPCT taifa Askofu Ezra  Ntamya amesema viongozi wanatakiwa kushirikiana na kujenga umoja na mshikamano ili kufikia malengo miongoni ikiwa ni kuendelea kuimirisha umoja na kutatua migogoro katika jamii.

Sauti ya Askofu wa Kanisa la PMC Ezra  Ntamya

Baadhi ya wajumbe ambao ni viongozi wa dini wameleza matumaini yao kwa viongozi ambao watashika nafasi hizo katika kufikia malengo ya CPCT Mkoa wa Kigoma.

Sauti ya Baadhi ya wajumbe ambao ni viongozi wa dini

Uchaguzi huo umelenga kuleta uongozi mpya utakaoliongoza vema kundi hilo la makanisa ya Kipentekoste katika kutekeleza malengo yake ya Kiroho na kijamii kwa maendeleo ya mkoa na taifa kwa ujumla.

Askofu Mkuu wa Kanisa la PMC na njumbe wa Halmashauri kuu ya CPCT Taifa, Picha na Hagai Ruyagila