Joy FM

Kasulu yaimarisha usafi kuepuka magonjwa ya mlipuko

30 July 2025, 13:04

Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Kasulu Mwl. Vumilia Simbeye akiwa katika zoezi la usafi, Picha na Hagai Ruyagila

Usafi na mazingira ni jambo muhimu katika maisha ya binadamu ambapo usafi humaanisha hali ya kuwa safi kimwili, nyumbani, shuleni, na katika maeneo ya kazi.

Na Hagai Ruyagila

Uwepo wa vyombo maalumu vya kuzoa taka katika Halmashauri ya mji wa Kasulu Mkoani Kigoma unatajwa kuimarisha hali ya usafi na utunzaji wa mangira katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.

Vifaa hivyo ambavyo hutumiwa na kikundi cha wahifadhi usafi mazingira katika halmashauri ya mji wa Kasulu umeleta matokeo chanya katika suala zima la utunzaji wa mazingira kutokana na elimu ambayo wananchi wanapatiwa.

Mwenyekiti wa kikundi hicho Bw. David Mathew amesema kauli mbiu yao ya Taka sifuri afya Bora imewaibua wananchi wengi katika kuimarisha hali ya usafi wa mazingira katika maeneo yao ukilinganisha na hali ilivyokuwa hapo awali wakati likitumika gari maalumu la kubeba taka.

Sauti ya Mwenyekiti wa kikundi hicho Bw. David Mathew
Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Kasulu Mwl. Vumilia Simbeye akishiriki zoezi la usafi wa mazingira, Picha na Hagai Ruyagila

Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Kasulu Mwl. Vumilia Simbeye amesema kwasasa mji huo umeendelea kuimarika katika suala la usafi kupitia vifaa hivyo vya kuzoa taka ukiwa ni mwezi mmoja umepita tangu kampeni ya usafi wa mazingira kuzindunduliwa mwishoni mwa mwezi juni.

Sauti ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Kasulu Mwl. Vumilia Simbeye

Baadhi ya wananchi wanashauri serikali kulivalia njuga suala hilo na kuchukua hatua kwa wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao Usafi ili kuwanusuru na magonjwa ya mlipuko.

Sauti ya wananchi Kasulu

Kaimu mkuu wa kitengo udhibiti wa taka na usafi wa mazingira Malagera Lukiko amesema wameanza kubuni mbinu bora za kuwafikia wananchi wengi kwa ajili ya kutoa Elimu.

Sauti ya Kaimu mkuu wa kitengo udhibiti wa taka na usafi wa mazingira Malagera Lukiko