Joy FM
Joy FM
30 July 2025, 11:57

Vijana waliohitimu mafunzo katika chuo cha veta Kigoma wametakiwa kutumia ujuzi walioupata kuchangamkia fursa zilizopo kujiajiri.
Na Orida Sayon
Waziri wa maendeleo ya jamii, wanawake, jinsia na makundi maalumu Mh. Doroth Gwajima ameelekeza wakurugenzi wa maendeleo ya jamii nchini kupeleka wadau maendeleo katika vyuo vya ufundi stadi veta kutoa elimu ya fursa kwa wanafunzi.
Waziri Doroth Gwajima ametoa maagizo hayo wakati wa ziara iliyofanyika katika chuo cha ufundi stadi veta kigoma iliyolenga kuwatunuku vyeti wahitimu wa kozi za muda mfupi na kutembelea ofisi ya dawati la jinsia VETA Kigoma ikiwa ni moja ya utekelezaji wa mradi wa wezesha binti unaofadhiliwa na shirika la Enabel.
Aidha waziri Gwajima amewataka vijana kutumia ujuzi waliopata kama chanzo cha kujipatia ajira na kuajiri kwa manufaa yao familia huku wakipinga kila aina ya ukatili na matumizi ya dawa za kulevya.
Mkurugenzi Mkazi wa enabel nchini Tanzania Bw. Koenraad Geonkint amesema Kiasi cha shilingi billion 3 za kitanzania zimewekezwa kusaidia programa ya mafunzo ya ufundi katika vyuo vya ufundi stadi ili kuwezesha vijanaa zaidi ya 2300 kupata mafunzo ya ujuzi Mkoani Kigoma.
Baadhi ya wahitimu waliotunukiwa vyeti vya kozi za muda mfupi akiwemo Asha Omary Mohammed wanaeleza namna ujuzi utakavyowanufaisha.