Joy FM

“Polisi jamii isaidie kupunguza matukio ya ukatili Kigoma”

25 July 2025, 14:26

Mkuu wa Polisi Jamii Wilaya ya Kigoma SP. Nganda Masumbuko akizungumza katika mkutano wa hadhara, Picha na Hamis Ntelekwa

Polisi jamii ni nguzo muhimu katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili na kupitia ushirikiano wa karibu na jamii, elimu, na ufuatiliaji wa karibu, wanasaidia kupunguza ukatili na kukuza mazingira salama na yenye haki kwa wote.

Na Josephine Kiravu

Kufuatia kukithiri kwa matukio ya ukatili kwa watoto, Mkuu wa Polisi Jamii Wilaya ya Kigoma SP. Nganda Masumbuko ameagiza kuanzishwa kwa vikundi vya polisi jamii ili kudhibiti matukio hayo ambayo yamekuwa yakileta athari kwa watoto.

Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Kagera SP. Masumbuko amesema ikiwa kila mtaa wataanzisha vikundi vya polisi jamii itapunguza kwa kiasi kikubwa matukio ya uhalifu pamoja na ukatili.

Sauti ya Mkuu wa Polisi Jamii Wilaya ya Kigoma SP. Nganda Masumbuko
Wananchi wa Kata ya Kagera wakiwa katika mkutano wa hadhara, Picha na Hamis Ntelekwa

Na hapa Afisa ustawi wa jamii kata ya Kagera Shani Kassim anatoa wito kwa wazazi na walezi kuwafanya marafiki watoto ili kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya ukatili.

Sauti ya Afisa ustawi wa jamii kata ya Kagera Shani Kassim

Hata hivyo wananchi wa kata ya Kagera wamekiri uwepo wa vitendo vya ukatili kwenye maeneo yao huku wakihitaji elimu zaidi itolewe ili kuwanusuru watoto ambao ni waathirika wa vitendo hivyo.

Sauti ya wananchi wa kata ya Kagera

Licha ya adhabu ambazo zimekuwa zikitolewa kwa wanaobainika kufanya ukatili kwa watoto lakini bado matukio hayo yameendelea kuripotiwa mengine yakiwahusisha wazazi kuwabaka watoto wao wa kuwazaa.

Hakika ni jukumu letu sote kuhakikisha tunatokomeza vitendo vya ukatili kwa kupaza sauti na kuwafichua wanaotekeleza vitendo hivyo.