Joy FM
Joy FM
23 July 2025, 16:05

Wasafiri wametakiwa kutoa taarifa za uvunjifu wa amani wakati wakiwa safarini.
Na Hagai Ruyagila
Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama barabarani Wilayani Kasulu limetoa wito kwa wasafiri wote wanaotoka Wilaya hiyo kuelekea maeneo mengine kutoa taarifa mapema wanapobaini dalili zozote zinazoashiria uvunjifu wa amani au hatari yoyote inayoweza kuhatarisha usalama wao wakiwa safarini.
Wito huo umetolewa na Mrakibu wa Polisi DTO Patrick Damas ni mkuu wa usalama barabarani Wilayani Kasulu wakati akitoa elimu kwa wananchi kupitia vyombo vya habari ofisini kwake.
Aidha DTO Afande Damas amewashauri wananchi kuhakikisha wanakuwa na mawasailiano ya moja kwa moja na askari ili kurahisisha utoaji wa taarifa pindi hali ya dharura au tukio la kihalifu linapotokea.
Baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Kasulu wamesema kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pindi watakapoona au kuhisi vitendo vya uvunjifu wa amani vinatokea wawapo safarini au sehemu yoyote ni vizuri maana itasaidia hatua ziweze kuchukuliwa kwa haraka.