Joy FM
Joy FM
21 July 2025, 15:44

Wajasiriamali wakubwa na wadogo pamoja na wafanyabiashara zaidi ya 100 wamepatiwa elimu ya uwekezaji mitaji.
Na Emmanuel Matinde
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dkt. Rashid Chuachua, amehimiza jamii kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba pamoja na kufundisha kizazi cha sasa umuhimu wa kujiwekea akiba ikiwa ni pamoja na kuwekeza fedha kwenye mifuko rasmi ya uwekezaji inayotambulika kwa ajili ya manufaa ya baadaye.
Dkt. Chuachua, amesema hayo akiwakilishwa na Afisa Tawala Wilaya ya Kigoma, Maximilian Ngasa, kwenye kongamano la uwekezaji lililolenga kutoa elimu ya uwekezaji hususani kwenye mifuko ya uwekezaji wa pamoja.
Kongamano hilo limeandaliwa na UTT Amis, kwa kushrikiana na wadau wengine, ambapo Afisa Masoko Mwandamizi kutoka UTT Amis, Raheem Mwanga, amesisitiza kwa jamii kutumia mifuko ya uwekezaji kama sehemu salama ya kuwekeza na kukuza mitaji yao.
Baadhi ya washiriki wamezungumzia kongamano hilo kuwa lenye faida kubwa kwao wakilenga kutumia fursa hiyo kwa manufaa yao ya baadaye.