Joy FM

RC Kigoma ataka juhudi ukusanyaji mapato kuongezeka

9 July 2025, 15:35

Watumishi wa halmashauri ya Wilaya Kasulu wakiwa katika mkutano na mkuu wa Mkoa Kigoma, Picha na Hagai Ruyagila

Ukusanyaji wa mapato unatajwa kuchochea maendeleo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Na Hagai Ruyagila

Mkuu wa mkoa wa Kigoma IGP Mstaafu Balozi Simon Sirro amewataka wakusanyaji wa mapato katika Wilaya ya Kasulu kutoka katika halmashauri zote za wilaya ya kasulu kutumia njia bora za ukusanyaji wa mapato ili kuepuka vurugu.  

Balozi Sirro ametoa wito huo wakati akizungumza na watumishi wa umma kutoka idara mbali mbali, viongozi wa dini, kamati ya ulinzi na usalama pamoja na viongozi wa vyama vya siasa katika wilaya ya Kasulu.

Amesema mapato ndiyo msingi wa maendeleo ya wilaya na taifa kwa ujumla hivyo ni vizuri kutoruhusu uchaguzi mkuu wa mwaka huu kuwa kikwazo katika ukusanyaji wa mapato.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Kigoma IGP Mstaafu Balozi Simon Sirro

Katika hatua nyingine Balozi Sirro amewataka wananchi wa wilaya ya Kasulu kudumisha amani na utulivu kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi oktoba mwaka huu ambapo wananchi watapata ridhaa ya kuchagua madiwani, wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ameendelea kusema kuwa ni muhimu kampeni za uchaguzi zifanyike kwa amani, weledi na kuzingatia sheria na utaratibu, Pia amebainisha kuwa serikali imejipanga kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa uhuru na haki kwa pande zote.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Kigoma IGP Mstaafu Balozi Simon Sirro

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa wafanyabiashara wilaya ya kasulu Bryton Baliko ameiomba serikali kuhusiana na wafanyabiashara ikiwa ni pamoja na kushirikiana katika mabadiliko yoyote yanayotokea kwa mlipa kodi kabla ya kuanza utekelezaji ili kuepuka migogoro baina ya serikali na wafanyabiashara.

Sauti ya Mwenyekiti wa wafanyabiashara wilaya ya kasulu Bryton Baliko