Joy FM
Joy FM
9 July 2025, 09:51

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Kigma limewataka wananchi kuendelea kuchukua hatua za kukabiliana na majanga ya moto ambayo yanaweza kujitokeza katika maeneo yao.
Na Esperance Ramadhan
Baadhi ya Wananchi Mkoani Kigoma wamepatiwa elimu ya kuzima moto pindi linapotokea tatizo la moto na kuhakikisha wanachukua tahadhari ilikunusuru majanga yanayoweza kujitokeza ikiwemo vifo .
Akizungumza na wananchi wa kata ya Kigoma mjini Manispaa ya Kigoma Ujiji Mrakibu Msaidizi Michael Maganga ambaye pia ni kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Kigoma amesema elimu waliyoitoa ya kuzima moto ni mbunu za kujiokoa waowenyewe pindi tukio la moto linapotokea.

Naye Mkaguzi Bahati Salum ambaye pia ni Mkuu wa mkitengo cha usalama dhidi ya majanga ya moto Mkoani Kigoma amesema wataendelea kutoa eluimu kwa wananchi ili kuondoa hali ya taharuki pindi majanga ya moto inapotokea.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wameeleza namna wanavyochukuwa tayari kukabiliana na majanga ya moto hasa kwenye maeneo ya mkusanyiko.