Joy FM
Joy FM
3 July 2025, 15:15

Mkuu wa Mkoa Kigoma Simon Srro amesema atashirikiana na viongozi na wananchi wa Mkoa Kigoma katika kuhakikisha maeneleo ya Mkoa yanasonga mbele.
Na Lucas Hoha
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali Mstaafu wa jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye amekabidhi ofisi kwa Mkuu wa Mkoa mpya Inspekta Jenerali Mstaafu IGP Balozi Simon Sirro kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Andengenye amesema mkoa wa Kigoma anauacha ukiwa katika hali ya utulivu, huku akitaja mafanikio yaliyopatikana ikiwemo serikali kutoa Shilingi Trioni 11 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Inspekta Jenerali Mtaafu IGP, Balozi Simon Sirro amesema amepokea maelekezo ya kuendeleza mipango ya kuufungua mkoa wa kigoma kwani ni mkoa wa kimkakati kiuchumi.
Na hawa ni baadhi ya viongozi mbalimbali walioshiriki kwenye hafla hiyo akiwemo balozi wa ubalozi mdogo wa Burundi Mkoani Kigoma amesema wataendelea kutoa ushirikiano kwa mkuu wa Mkoa mpya ikiwemo kuendeleza ujirani mwema.
Kabla ya kustaafu, Andengenye amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kwa muda wa miaka 5 tangu ateuliwe Julai 2020 na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Hayati John Magufuli akichukua nafasi hiyo kutoka kwa Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga.
