Joy FM
Joy FM
2 July 2025, 16:01

Benki Kuu ya Tanzania imeendelea kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kuzingatia matumizi na utunzaji bora wa fedha.
Na Mwandishi wetu Uvinza
Wakulima Mkoani Kigoma wametakiwa kuachana na utamaduni wa kuhifadhi fedha ndani na badala yake kutumia huduma za kibenki ili kuondokana na adha ya upotevu wa fedha ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara.
Kaimu Meneja Msaidizi idara ya huduma jumuishi za fedha kutoka Benki kuu ya Tanzania BOT Edmund Mbokosi amesema kumekuwa na utamaduni wa baadhi ya wakulima hususani maeneo ya vijijini kuhifadhi fedha kwa kuzichimbia chini jambo ambalo si salama.
Na hapa wakulima nao wanaeleza ni kwa namna gani uhifadhi wa fedha kwa njia ya kienyeji umekuwa ni mwiba kwao.
Kwa upande wake, Mchumi kutoka Benki kuu ya Tanzani Lucas Magazi amesema wakulima wanatakiwa kuachana na mikopo umiza ambayo imekuwa ikiwarudisha nyuma kila kukicha.
Kwa pande wake, Afisa mtendaji kata ya Kalya Jeremaya Fanueli amesema elimu waliyopatiwa itasaidia kwa kiasi kikubwa kuwaondoa wananchi kwenye changamoto ya mikopo umiza.