Joy FM
Joy FM
26 June 2025, 16:12

Ulemavu ni hali ya kuwa na hitilafu ya kudumu mwilini au akilini, inayomzuia mtu kutekeleza shughuli fulani katika maisha yake tofauti na watu wengine lakini watu wenye ulemavu wakiwekewa mazingira rafiki kulingana na hitilafu zao wanaweza kutimiza majukumu yao kama mtu asiye na ulemavu.
Na Tryphone Odace
Wazazi na walezi Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wametawaki kutowaficha watoto wao wenye mahitaji maalumu hususan wenye ulemavu na baadala yake wametakiwa kuwapeleka shule ili waweze kupata elimu itakayowasaidia kutimiza ndoto zao.
Wito huo umetolewa na Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kabanga Mazoezi, Bi. Happiness Boyi wakati akizungumza na Rradio Joy fm ambapo amesisitiza umuhimu wa jamii kutambua na kuthamini machango wa watoto wenye mahitaji maalumu.
Aidha Mwl. Boyi Ametoa shukrani kwa serikali kuendelea kuwawezesha watu wenye mahitaji maalumu hususan katika kuwapatia chakula na mahitaji mengine ya msingi shuleni.
Baadhi ya Wazazi na Walezi wa watoto wenye mahitaji maalumu kutoka Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wamesema watoto hao wanayo haki ya kupata elimu kama ilivyo kwa watoto wengine, na hivyo hawapaswi kufichwa majumbani.

Wito huo unalenga kuhamasisha ushiriki wa watoto wote katika elimu bila ubaguzi, sambamba na kuhakikisha kuwa haki ya elimu kwa watoto wenye ulemavu inatekelezwa kwa vitendo katika jamii.