Joy FM
Joy FM
4 June 2025, 15:59

Rushwa ya ngono ndani ya vyombo vya habari, hujumuisha kubadilishana tendo la ngono na ajira, au tendo la ngono na uhakika wa usalama wa kazi na wakati mwingine upendeleo katika kuchapishwa kwa habari.
Utafiti uliochapishwa mwaka 2022 na Shirika la Habari la Kimataifa (WAN-INFRA) ulibaini asilimia 41 ya wanahabari wanawake wamewahi kupitia unyanyasaji wa kingono au wa kihisia katika maeneo yao ya kazi lakini kati ya hao, ni mmoja tu kati ya watano aliyeripoti kesi za unyanyasaji huo.