Joy FM

Wanaume ni vichwa na viongozi kuweni kielezo cha kanisa Kasulu

26 May 2025, 16:03

Paroko wa Parokia ya Mrubona Kasulu mjini Padre Gaspa Balkumutwe, Picha na Emmanuel Kamangu

Wanapokutana wanaume wakatoliki na kufanya hafla mbali mbali ni moja ya kuendelea kujenga  umoja  ikiwemo  kutiana moyo katika kuendelea kushiriki matendo ya huruma kwa kuwatunza wahitaji wenye shida mbalimbali”

Na Mwandishi wetu

Wanaume wa kanisa katoliki parokia ya mrubona jimbo  katoliki la kigoma wametakiwa kuwa kielelezo cha kanisa ikiwemo kusimama imara katika kulifanya kanisa kuwa na umoja.

Amesema hayo, Paroko wa Parokia ya Mrubona kasulu mjini Padre Gaspa Balkumutwe katika misa takatifu ambayo imeambatana na sherehe za utume wa wanaume wa katolki Uwaka  parokiani apo ambapo ameleleza kuwa kanisa linahitaji wanaume wa kutosha na  wenye moyo thabiti  wa kulitunza kanisa la Mungu.

Sauti ya Paroko wa Parokia ya Mrubona kasulu mjini Padre Gaspa Balkumutwe

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa wanaume wa katoliki Uwaka Parokia ya Mrubona Bw Camilius Tomas amesema wanapokutana wanaume wakatoliki na kufanya hafla mbali mbali ni moja ya kuendelea kujenga  umoja  ikiwemo  kutiana moyo katika kuendelea kushiriki matendo ya huruma kwa kuwatunza wahitaji wenye shida mbali mbali.

Mwenyekiti wa wanaume wa katoliki Uwaka Parokia ya Mrubona Bw Camilius Tomas

Nao baadhi ya wanaume wakatoliki ambao wameshiriki katika kutaniko hilo wamesema wamepokuwa na sherehe za mara kwa mara za uwaka huwasaidia kukua kiimani pamoja kuwavuta  wanaume wengi zaidi kuingia katika utume huo.

Sauti ya baadhi ya wanaume wakatoliki ambao wameshiriki katika kutaniko hilo
Ni baadhi ya wanaume wakatoliki ambao wameshiriki katika kutaniko hilo, Picha na Emmanuel Kamangu

Hata hivyo wanaume hao wakatoliki wameongeza kuwa wanawajibu wa kuchochea maendeleo ya kanisa .