Joy FM
Joy FM
21 May 2025, 14:37

Ni kosa la kisheria kunukuu, kutangaza au kubainisha bei kwa kutumia fedha za kigeni, kulazimisha, kuwezesha au kupokea malipo kwa fedha za kigeni.
Na Glory Paschal
Benki kuu ya Tanzania BoT imesema malipo yote ya bidhaa na huduma yanapaswa kufanyika kwa kutumia shilingi ya Tanzania lengo ikiwa ni kuongeza thamani fedha ya ndani.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Masoko ya Fedha BoT, Bw. Emmanuel Akaro, wakati akizungumza katika semina ya waandishi wa habari iliyofanyika katika ofisi za Benki Kuu jijini Dar es Salaam, kuhusu Kanuni za Matumizi ya Fedha za Kigeni za Mwaka 2025.
Amesema kwa mujibu wa Kanuni hizo, bei na malipo ya bidhaa na huduma zote ndani ya nchi yanapaswa kufanyika kwa Shilingi ya Tanzania.
Amesema ni kosa la kisheria kunukuu, kutangaza au kubainisha bei kwa kutumia fedha za kigeni, kulazimisha, kuwezesha au kupokea malipo kwa fedha za kigeni, au kukataa malipo yanayofanyika kwa shilingi ya Tanzania.