Joy FM
Joy FM
9 May 2025, 12:54

Serikali imesema itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wakulima wa pamba ili waweze kulima pamba kwa wingi.
Na Hagai Ruyagila
Wakulima wa zao la pamba wilayani Kasulu, mkoani Kigoma, wameiomba serikali kuongeza bei ya ununuzi wa zao hilo ili wakulima waweze kuzalisha kwa wingi.
Katika taarifa ya maendeleo ya uzalishaji wa pamba ambayo imetolewa na viongozi wa AMCOS mbalimbali halmashauri ya wilaya ya Kasulu wamesema bei ya sasa ni ndogo na imesababisha baadhi ya wakulima kukata tamaa ya kuendelea na zao hilo la Biashara na kulazimika kuhamia kwenye mazao mengine.
Efraimu Erasto katibu wa Buyonga Amcos ni miongoni mwa viongozi wa AMCOS wanaeleza baadhi ya changamoto zinazowakabili katika kilimo cha zao la pamba huku suala la Bei likitakiwa kutazamwa kwa jicho la tatu.
Meneja wa Kampuni inajihusisha na ununuzi wa pamba katika Wilaya ya Kasulu ambayo ni Uvinza Ginnery, Bw. Mabula William, amesema kampuni hiyo ina uhitaji mkubwa wa zao hilo kutokana na mahitaji ya viwanda hivyo wameweka mikakati ya kuongeza bei ya zao hilo.

Akizungumzia kuhusu zao la pamba, Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Isaac Mwakisu, amesema kwa kushirikiana na mnunuzi wa zao hilo wataangalia uwezekano wa kuongeza bei, kwa lengo la kuhakikisha wakulima wananufaika na zao la pamba.

Mkaguzi wa pamba wilaya ya Kasulu Michael Kihiga amesema uwepo wa maafisa ugani wa BBT umeweza kusajili kwenye mfumo wakulima 671wenye jumla ya Ekari 2977.16