Joy FM

Kilio kisichosikika utelekezaji watoto Kigoma

8 May 2025, 13:56

Kwa mujibu wa Takwimu za Ofisi ya Ustawi wa Jamii, kati ya mwezi March hadi April mwaka 2025 pekee kuna zaidi ya watoto 150 walitelekezwa katika Wilaya ya Kigoma. Hii leo wengi wa watoto hawa wanaishi mtaani, hawawajui wazazi wao huku wakikumbwa na adha za kimwili, kiafya na hata kiakili wanapoishi katika mazingira magumu mtaani.

Mwandishi wetu Winfrida Ngassa amekuandalia makala haya baada ya kuwatembelea watoto hao na kuzungumza na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na watumishi wa Serikali na wataalamu wa Saikolojia.