Joy FM

Mvua yaua watoto wawili, kaya 60 zajaa maji Kigoma

21 April 2025, 11:32

Barabara ya Kibirizi ikiwa imefurikwa na maji watu wakivuka kutumia mtumbwi-Picha na Hamisi Ntelekwa

Mabadiriko ya tabianchi yamepelekea mvua nyingi kunyesha katika maeneo mbalimbali ambapo mwaka 2023, zilisababisha  nyumba zaidi ya mia moja sabini, kuvamiwa na maji huku zikiacha madhara na mwaka huu zimesababisha vifo vya watoto wawili

Na Kadislaus Ezekiel

Mvua Zinazoendela Kunyesha Mkoani Kigoma, zimepeleka watoto wawili kufariki kwa kusombwa na maji katika kata ya Kibirizi, huku kaya zaidi ya sitini zikivamiwa na maji Katika mitaa ya Mwanga Majengo na Katubuka Manispaa ya Kigoma ujiji, na waathirika wakizidi kuililia serikali kuchukua hatua za haraka ikiwemo kuondoa maji yanayozidi kuvamia makazi ya watu.

Kwa mvua ambayo imenyesha tena kwa zaidi ya masaa sita, imeongeza madhara na kusababisha kaya zingine sitini kukumbwa na mafuriko hekaheka za kuhama zikiendelea kwa familia zilizovamiwa na maji, na Kujaribu kuokoa baadhi ya vitu kutoka kwenye nyumba zao.

Sauti za wananchi wakieleza hali ya maji kwenye makazi yao

Kufuatia makazi ya watu kuvamiwa na Maji na kukosa makazi, hifadhi ya wananchi hawa wanaamua kuweka kambi katika shule ya msingi majengo, huku kilio chao ni kilekile cha kuiomba serikali kutafuta suluhu ya kuondoa maji haya.

Sauti za wananchi

‎Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya inafika kuzungumza na wahanga hawa kubwa ikiwataka kuwa na subira wakati serikali ikishughulikia changamoto hii.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Kigom Dkt Chuachua