Joy FM
Joy FM
15 April 2025, 13:36

Vitendo vya uhalifu vinaweza kudhibitiwa iwapo tu wananchi watashirikiana na Polisi kata kukabiliana na vitendo vya uhalifu kwenye jamii
Na Emmanuel Kamangu
Polisi kata wilayani kasulu wametakiwa kushirikiana kikamilifu na wananchi katika kata wanazoziongoza ili kuwa rahisi kubaini wahalifu.
Amebainisha hayo Mkaguzi msaidizi wa polisi wille Lupa ambaye pia ni mratibu wa polisi jamii wilaya ya kasulu wakati akizungumza na redio joy juu ya majukumu ya polisi kata na kueleza kuwa wanawajibu wa kuhakikisha wanakuwa chanzo cha kuhamasisha maendeleo katika kata husika.
Aidha Lupa amesema kuwa polisi kata nje na mambo mengine anatakiwa kuhakikisha kila jambo katika kata yake linalohatarisha usalama wa raia na mali zao analitambua kwa wakati na kulishugulikia kwa ajili ya kuimalisha utulivu na amani.
Hata hivyo Lupa amewataka wananchi wa wilaya ya kasulu kuhakikisha wanawapa ushirikiano wa kutosha polisi kata sambamba na polisi jamiii ili kuwa rahisi kutanzua vitendo vya uharifu katika maeneo yao.