

27 March 2025, 11:01
Serikali imeendelea kuhakikisha upatikanaji wa maji unakuwa mkubwa kwa wananchi wilayani Buhigwe.
Na Kadislaus Ezekiel
Wananchi wa vijiji 8 vya Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, wameomba serikali kusimamia wakandarasi wanaojenga miradi ya maji ili kuharakisha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama, hatua inayotazamwa na wananchi kutatua migogoro ya ndoa kwa kufuata huduma hiyo umbali mrefu na kutumia muda mwingi, kwa kufuata maji ya mito na visima.
Kwa sasa Wilaya ya Buhigwe kupitia Wakala wa maji na usafi wa mazingira RUWASA, wanasimamia Miradi ya maji mikubwa miwili ambayo kwa ujumla inaghalimu zaidi ya bilioni 14 na imeanza kutoa huduma ya maji safi na salama kwa baadhi ya vijiji vinavyohusika.
Wananchi wakiwa katika ukaguzi wa miradi hiyo pamoja na Viongozi, wamesema kukamilika miradi hiyo ni utatuzi mkubwa wa migogoro ya ndoa, na kupata huduma ya uhakika ya maji safi na salama.
Akitoa ufafauzi wa mradi wa maji unaokuja kutatua changamoto ya maji katika vijiji nane, Kwa thamani ya zaidi ya Bilioni 9, Meneja wa Wakala wa maji na usafi wa mazingira RUWASA Wilaya ya Buhigwe Gordeni Katoto, amesema umefiakia asilimia 65 na umeanza kutoa huduma ya maji kwa baadhi ya Vijiji.
Kuhusu Mradi wa Bilioni Tano ambao upo chini TANROADS kupitia Ujenzi wa Barabara ya Manyovu Kasulu wenye thamani ya Bilioni 5.1, amesema upo asilimia 21, huku mkuu wa wilaya ya Buhigwe Kanali Mstafu Michael Ngayalina akisisitiza miradi kukamilika.